HabariMilele FmSwahili

William Ruto aionya mahakama dhidi ya kushawishiwa na upinzani

Naibu rais William Ruto ameendelea kuionya idara ya mahakama dhidi ya kushawishiwa na upinzani katika maamuzi yake hasaa kuhusu matayarisho ya uchaguzi. Akizungumza huko Lodwar kaunti ya Turkana wanakosaka kura na rais Uhuru Kenyatta, naibu rais anasema ni vyema kwa idara hiyo kuheshimu Uhuru wake na kufanya  maamuzi ikizingatia wakenya  wala sio watu binafsi. Ameunga mkono haja iliyotolewa na katibu wa Jubilee Raphel Tuju, kuwa idara hiyo inafaa kuchunguzwa kwa kina kuwatambua majaji walio na uhusiano wa karibu na baadhi ya viongozi wa upinzani.

Show More

Related Articles