HabariMilele FmSwahili

Jubilee yasema haitakubali tarehe ya uchaguzi kubadilishwa

Chama cha Jubilee kinasema hakitakubali mdahalo wowote wa kubadili tarehe ya uchaguzi. Wakizungumza katika kikao cha wagombea urais na IEBC, wawakilishi wa rais Uhuru Kenyatta wamekosoa mkao huo. Seneta Kithure Kindiki amesema IEBC inapaswa kupewa uhuru wake wa kutafuta mwanakandarasi mwingine bila muingilio wa wagombea hao.Akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya mgombea wa NASA Raila Odinga, Seneta James Orengo alisisitiza wako tayari kwa uchaguzi akionya IEBC dhidi ya kutumia suala la kuchapisha karatasi za urais kupendekeza kuhairishwa uchaguzi.Nao wagombea urais Ekuru Aukot na Abduba Dida, waitaka IEBC kutoa hakikisho kuhusu mfumo wake wa kutangaza matokeo na teknoljia itakayotumiwa katika uchaguzi huo.Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati naye amekariri licha ya IEBC kuwa tayari kwa uchaguzi, uamuzi wa kuwaagiza kutoa upya kandarasi ya kuchapisha karatasi za kura ya urais ni changamoto kuu kwa sasa.

Show More

Related Articles