HabariMilele FmSwahili

NASA yadai wapiga kura 400,865 wamejisajili zaidi ya mara moja

Mrengo wa NASA sasa unadai kuwepo kwa wapiga kura  400,865 ambao wamejisajili zaidi ya mara moja. NASA inasema wapiga kura hao ni kutoka kaunti  tofauti, maeneo   bunge na wadi mbali mbali. Mrengo huo sasa umeapa kuiandikia tume ya uchaguzi ya IEBC kuhusu suala hilo. Mrengo huo sasa unataka kuchapishwa kwa sajili yote ya wapiga kura na kutaka kupigwa msasa zaidi kwa sajili yenyewe. Mrengo wa NASA  umekuwa ukitilia shaka ukaguzi wa sajili ya wapiga kura  uliioendeshwa na  kampuni   ya KMPG . Wana NASA wameibua madai hayo kwenye kampeni zao eneo la Pwani.

Show More

Related Articles