HabariMilele FmSwahili

Jubilee yataka majaji kuchunguzwa

Viongozi wa Jubilee sasa wanataka uchunguzi wa kina kuendeshwa katika idara ya mahakama ili kuwatambua majaji walio na uhusiano wa karibu na baadhi ya viongozi wa upinzani. Katibu wa Jubilee Raphael Tuju anasema jaji George Odunga aliyeshiriki jopo la majaji 3 liliotoa uamuzi wa kuchapishwa upya karatasi za kura ya urais amemuoa binamuye seneta wa Siaya James Orengo na ambaye ni wakili wa NASA.Seneta wa Elgeyo Marakwet naye anamtuhumu mkuu wa chama cha mawakili nchini kwa kumtetea Odunga akisema hata yeye ana mahusiano ya karibu na muungano wa NASA kwa upande wake kiongozi wa Jubilee bungeni Adan Dualle anasema kamwe hawatokubali upinzani kushinikiza kubuniwa serikali ya muungano kutokana na  NASA kuibua madai yanayoweza kuibua vurugu nchini

Show More

Related Articles