HabariMilele FmSwahili

Wanajeshi walipua msitu wa Boni kuwaondoa waasi wa Alshabaab

Wanajeshi wa KDF wanaendelea  kurusha mabomu ya angani  katika msitu wa Boni katika juhudi za  kuwaondoa waasi wa Alshabaab wanaoendesha shughuli zao kwenye msitu huo. Shirika la msalaba mwekundu kwa ushirikiano na maafisa wa serikali wanaendesha  shughuli ya kuwaondoa  wenyeji kuelekea maeneo salama. Wakati huo huo serikali  imewataka wanasiasa kutoingiza siasa kwenye marufuku ya miezi 3 iliyowekwa na  wizara ya usalama katika kaunti hiyo ya Lamu pamoja na kaunti ya Garissa na Tana river. Mshirikishi wa serikali eneo la Pwani Nelson Marwa  amewataka wenyeji kushirkiiana na maafisa wa usalama katika kutoa taarifa muhimu kufanikisha oparesheni hiyo.

Show More

Related Articles