HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanyamapori Watatiza Usalama Bamba.

Usalama eneo la Bamba kata ndogo ya Ganze unaendelea kuzorota kufuatia ongezeko la wanyamapori wanaozurura karibu na makazi ya wananchi kutafuta maji ya kunywa.

Mbunge wa eneo hilo Peter Shehe anasema wanyama hao wamekuwa tishio kwa usalama wa mwananchi  hasa kinamama na watoto, pale wanaoenda mtoni kutafuta maji.

Ameitaka serikali kuwapatia mafisa wa shirika la wanyamapori nchini KWS vifaa vya kutosha ili kuwawezesha kuwafurusha wanyama hao.

Naibu kamishina eneo hilo Mohammed Mwabudzo amesema ukosefu wa mabwawa ya maji porini ndio chanzo kikuu cha wanyama hao kufika katika maakazi ya wananchi, akiongeza kuwa tayari mikakati inawekwa ili kushughulikia tatizo hilo.

Show More

Related Articles