HabariPilipili FmPilipili FM News

Wabakaji Kusalia Kizimbani Mombasa.

Washukiwa wawili wamefikishwa katika mahakama ya shanzu hii leo Kwa tuhuma za ubakaji.

Salim Mohamed mwenye umri wa miaka 23 ameshtakiwa kwa tuhuma za kumbaka Mtoto wa miaka 7 maeneo ya Mshomoroni, huku mshukiwa mwengine Stephen ochieng mwenye umri wa miaka 23 , akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 12.

Wawili hao wamekana mashataka dhidi yao mbele ya hakimu Diana Mochache.

Kwa sasa wataendelea kuzuiliwa rumande, huku kesi yao ikitarajiwa kusikizwa mwishoni mwa mwezi huu wa saba.

 

Show More

Related Articles