HabariPilipili FmPilipili FM News

Tumeingia “Boni” Asema Marwa.

Magaidi wanaotumia msitu wa Boni katika kaunti ya Lamu kutekeleza mashambulizi katika kaunti hiyo wameonywa vikali wakati tayari serikali imeanza uvamizi ndani yam situ huo ili kukabiliana na magaidi hao.

Haya yamesemwa na mshirikishi mkuu wa serikali kuu kanda ya pwani Nelson Marwa wakati alipokutana na baadhi ya viongozi wa usalama kanda ya pwani mjini Mombasa.

Marwa amesema serikali inafanya juhudi kukabiliana na ugaidi katika sehemu hio huku akiwataka viongozi wa eneo hilo kutolitilia siasa swala la amri ya kutotoka nje iliotolewa na serikali.

Marwa ameongezea kuwa kama idara ya usalama kanda ya pwani watahakikisha amani inadumishwa msumu huu

 

Show More

Related Articles