HabariMilele FmSwahili

Wauguzi wakiri kutorudi kazini kabla mkataba wao kutiwa saini

Ukosefu wa fedha ndio umesababisha kutotiwa siani mkataba wa wauguzi wanaogoma. Tume ya kutathmini mishahara SRC imejitenga na madai inahujumu mkataba wa wauguzi, mwenyekiti Sarah Serem akisema mkataba huo ulibuniwa pasi na  kuzingatia uwezo wa kugharamia fedha hizo.Hata hivyo wauguzi hao wakiongozwa na naibu katibu Morrice Opetu wamekariri msimamo wao kuwa hawatarudi kazini kabla ya mkataba wao kutiwa saini. Opetu anasema wauguzi wako tayari kufungwa jela wakitetea haki yao.Misimamo hiyo inatolewa huku maandamano ya wauguzi yakishuhudiwa katika maeneo mbali mbali nchini.

Show More

Related Articles