HabariMilele FmSwahili

Jubilee yazidi kumshtumu jaji Maraga kwa kushirikiana na NASA

Chama cha Jubilee kimeendelea kumstuhumu jaji mkuu David Maraga kwa kutumiwa na upinzani kutatiza shughuli za IEBC. Katibu wa Jubilee Raphael Tuju anasema jaji Maraga alifaa kumuondoa jaji Odunga katika jopo la majaji 3 waliosikiza rufaa ya NASA kuhusiana na kesi ya uchapishaji karatasi za kura ya urais. Kulingana na Tuju jaji Odunga ana uhusiano wa karibu sana na wakili wa NASA  seneta James Orengo. Yakijiri hayo chama cha mawakili nchini LSK kimewaonya wanasiasa dhidi ya kutoa matamshi yanayoweza kutishia uhuru wa idara ya mahakama. Mwenyekiti Issac Okero amekosoa matamshi ya rais Kenyatta na naibu wake akidai yanakiuka haki za mahakama kikatiba na yanayoweza kuondoa imani ya umma katika idara hiyo.

Show More

Related Articles