HabariMilele FmSwahili

Mishahara ya watumishi wote wa umma kupunguzwa kuanzia mwaka ujao

Mishahara ya watumishi wote wa umma itapunguzwa kuanzia mwaka ujao. Ratiba ya hivi punde ya SRC inashirikia Rais atapokea shilingi milioni 1.44 kutoka milioni 1.6, huku naibu wake akipokea shilingi milioni 1.2. Magavana watapokea shilingi elfu 924 sawa na mawaziri huku waakilishi wadi wakipokea shilingi elfu 144 kama mshahara wao wa kila mwezi. SRC pia imefutilia mbali marupurupu ya usafiri na yale ya kuhudhuria vikao vya bunge kwa maseneta na wabunge ili kuhifadhi shilingi bilioni 8 zinazotumika zaidi gharamia mishahara ya watumishi hao.

Show More

Related Articles