HabariMilele FmSwahili

COTU yakosoa hatua ya Rais na naibu wake kuikashifu mahakama

Muungano wa COTU umekosoa hatua hatua ya rais Kenyatta na naibu wake kuikemea idara ya mahakama kufuatia uamuzi wake kuhusiana uchapishaji karatasi za kura ya urais. Katibu mkuu Francis Atwoli amesema kuishutumu mahakama huenda kukaondoa imani ya umma katika idara hiyo. Amesema Rais pamoja na viongozi wasioridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama kuu kusimamisha kandarasi ya kuchapisha karatasi za kura wanapaswa kukata rufaa.

Show More

Related Articles