HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta afuta deni la billion 1.5 lililokuwa linadaiwa wakulima Kajiado

Rais Uhuru Kenyatta amefuta deni la shilingi bilioni 1.5 lililolukuwa linadaiwa wakulima katika kaunti za Kajiado, Narok na Baringo na shirika la AFC. Katika taarifa msemaji wa ikulu Manoah Esipisu amesena rais ameiagiza wizara ya fedha kwa ushirikiano na shirika la AFC kuhakikisha wakulima hao wanarejeshewa hati miliki walizotumia kupata mikopo. Amesema rais Kenyatta pia atafuta deni linalodaiwa wakulima katika kaunti ya Samburu atakapozuru kaunti hiyo hivi karibuni.

Show More

Related Articles