HabariMilele FmSwahili

Viongozi wa kiislamu Tanariver waitaka serikali kuondoa marufuku ya kutotoka nje

Viongozi wa kiislamu katika kaunti ya Tanariver sasa wanaitaka serikali kuondoa marufuku ya kutoka nje nyakati za usiku iliyowekwa kufuatia ongezeko la  mashambulizi yanayotekelezwa na washukiwa wa kundi la Al shabbab viongozi hao wamekosoa hatua ya kujumuisha Tana river kwenye orodha ya maeneo hatari wakidai kaunti hiyo haijashuhudia uvamizi. Mwenyekiti wa baraza la Maimam na wahubiri wa kiislamu kaunti hiyo Sheikh Musa amesisitiza kuwa kaunti hiyo imeshuhudia utulivu tokea gavana wa sasa Hussein Dado na rais Uhuru Kenyatta walipochukuwa mamlaka miaka minne iliyopita na hakuna sababu ya kuwekewa marufuku hiyo.

Show More

Related Articles