HabariMilele FmSwahili

Jubilee kupeleka kampeini zake kaunti ya Turkana

Rais Uhuru Kenyatta leo anaelekea kaunti ya Turkana kusaka kura uchaguzi unapokaribia. Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wataanza ziara hiyo katika eneo la Kakuma kabla ya kuelekea eneo la Lokitaung. Msafara wa jubilee umeratibiwa pia kuuzuru Lodwar kabla ya kukita kambi huko Lokichar ambako rais Kenyatta anatarajiwa kupigia debe rekodi yake ya maendeleo.Kwengineko vigogo wa NASA leo wanatarajiwa kukutana na makamishna wa IEBC kabla ya kuendelea na kampeni zao kesho katika kaunti ya Mandera.

Show More

Related Articles