HabariMilele FmSwahili

Maandalizi ya mazishi ya marehemu Nkaiserry kuanza leo

Maandalizi ya mazishi ya marehemu generali Joseph Nkaisery yanatarajiwa kuanza rasmi leo. Msemaji wa familia ya waziri huyo wa zamani wa usalama Saitoti Ole Maika anatarajiwa kutangaza tarehe rasmi ya mazishi kufuatia mkutano wa wazee wa jamii hiyo utakaoandaliwa nyumbani kwake huko Ilbisil kaunti ya Kajiado. Hayo yakijiri familia ya Nkaisery inasubiri ripoti kamili ya upasuaji wa mwili wa marehemu kubaini chanzo cha kifo chake. Viongozi tofauti wa kisiasa wanaendelea kutoa wito wa ripoti hiyo kuwekwa wazi kwa umma.

Show More

Related Articles