HabariMilele FmSwahili

NASA yasema haina nia ya kubadili tarehe ya uchaguzi

Viongozi wa mrengo wa NASA wamemjibu rais wakisisitiza kuwa hawana nia ya kubadili tarehe ya uchaguzi. Mgombea mwenza wa NASA Kalonzo Musyoka amekana  usemi wa Jubilee kuwa NASA imekuwa ikiibua lalama za kila mara kwa lengo la kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi. Anasema baada ya kuzuru eneo la Rift Valley mrengo wa NASA umeongeza kiwango cha uungwaji mkono.
Wakiongea kwenye ziara yao kaunti ya Kilifi kinara wa upinzani Raila Odinga ameahidi kuwa mrengo wa NASA utashughulikia  suala tata la ardhi hasa kwa wenyeji wa pwani iwapo watatwaa uongozi. Raila ameendelea kutuhumu serikali kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha.

Show More

Related Articles