HabariMilele FmSwahili

NASA yakosoa marufuku ya kutotoka nje iliyowekwa katika kaunti za lamu, Tanariver na Garissa

Viongozi wa mrengo wa NASA wamekosoa marufuku ya kutotoka nje ya miezi mitatu iliyowekwa na serikali katika kaunti za Lamu Garissa na Tana river. Vinara wa NASA Musalia Mudavadi na Moses  Wetangula wanadai marufuku hiyo haitasaidia kukabili mashambuli ya kundi la Al shabaab na kuwa haifai. Badala yake wanasema marufuku hiyo itaathiri  idadi ya wenyeji wa kaunti hizo watakaojitokeza kushiriki zoezi la uchaguzi mwezi ujao. Wakiongea huko magarini Kaunti ya Kilifi wanasema ni mapema zaidi kwa  kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiangi kuweka marufuku hiyo. Wamesisitiza haja ya  kuondolewa kwa wanajeshi wa Kenya  walioko  nchini Somalia.

Show More

Related Articles