HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Hatua za mwisho za Joseph Nkaiserry

Huku waKenya wakiomboleza kifo cha waziri wa usalama Joseph Nkaiserry, maswali chungu nzima yanazunguka mauaji yake haswa ikizingatiwa kuwa waziri huyu alikuwa mzima wa afya hapo jana na hata kuhudhuria hafla ya maombi ya kitaifa.
Nyumbani kwake katika eneo la Ilbisil kaunty ya Kajiado, biwi la simanzi lilitanda katika mkutano ambao waziri Nkaissery alitarajiwa kuhudhuria na kusimamia mchango.huku nyumbani kwake hakukuwa na shughuli zozote.
Katika makao yake rasmi katika eneo la Karen maafisa wa usalama walishika doria katika eneo hilo kwa madai kuwa eneo hilo ni la ushahidi.

Show More

Related Articles