HabariMilele FmSwahili

Uchunguzi wa kubauni kifo cha Nkaiserry bado unaendelea

Uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha aliyekuwa waziri wa usalama wa kitaifa meja jenerali mustaafu Joseph Nkaiserry. Maafisa kutoka kitengo cha uchunguzi wametumwa katika makao yake  eneo la Karen na ukumbi wa Bomas hapa Nairobi kuendesha uchunguzi huo. Taarifa za mapema zinaonyesha baada ya kuhudhuria maombi ya kitaifa katika bustani ya Uhuru park, mwenda zake alielekea katika afisi yake ilioko katika jumba la harambee kabla ya kuelekea Bomas. Rais Uhuru Kenyatta amesema walikua na mwenda zake mwendo wa saa tatu usiku ambapo walizungumzia mipangilio ya usalama ya mashindano ya riadha miongoni mwa chipukizi.

Show More

Related Articles