HabariMilele FmSwahili

IEBC Kuandaa kikao na wagombea urais wote Jumatatu

Tume ya uchaguzi IEBC itandaa kikao na wagombea wote wa urais siku ya Jumatatu kujadili hatima ya kuchapishwa karatasi za kupigia kura za urais. Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati anasema uamuzi huo umeafikiwa kuhakikisha wagombea urais wanaridhishwa na mikakati ya IEBC inaweka katika kuchapisha karatasi hizo. Katika kikao na wanahabari, Chebukati amesema IEBC itakata rufaa dhidi ya uamzi wa mahakama kuu kuhusu kushirikishwa kwa umma katika kutoa kandarasi ya kuchapisha karatasi hizo za kupigia kura.Chebukati anasema licha ya matukio hayo, mipangilio ya kuandaa uchaguzi Agosti nane inaendelea. Anasisitiza wataheshimu uamzi wa mahakama na kuwahakikishia wakenya kutarajia uchaguzi huru na haki.

Show More

Related Articles