HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi Bomet walalamika kutolipwa mshahara kwa miezi tatu

Wafanyakazi wa kaunti ya Bomet wametoa ilani ya mgomo ya siku saba kufuatia kukawia kwa maishahara yao kwa miezi mitatu sasa.Mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Jesca Langat anasema jitihada za
kuwasiliana na idara husika kuhusiana na swala hilo hazijafaulu.
Akiwahutubia wanahabari mjini Bomet, anaeleza kuwa hali hiyo imewaweka katika hali ngumu ba hawawezi tena kukimu jamii zao.
Bi Langat aidha amemsuta gavana Isaac Ruto kwa kutumia muda mwingi kupiga siasa huku akiongeza kuwa mgomo huo utawashirikisha wafanyakazi wote.

Show More

Related Articles