HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta na naibu wake wahairisha ziara yao kaunti ya Turkana

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamehairisha ziara yao kaunti ya Turkana hii leo. Viongozi hao waliratibiwa kuzuru maeneo ya Lodwar na Lokchar leo kwa mikutano ya kujipigia debe lakini safari hiyo imesitishwa. Hatua hii imetokana na kifo cha ghafla cha waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Ole Nkaissery aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo. Hata hivyo vigogo wa NASA wamesema wataendelea na ziara yao huko pwani. Wakiongozwa na Raila Odinga,wana NASA wanazuru maeneo toafuti kaunti ya Kwale kujipigia debe.

Show More

Related Articles