HabariMilele FmSwahili

Raila asema IEBC ina muda wakutosha wa kutoa upya kandarasi ya kuchapisha karatasi za kura

Mgombea urais wa muungano wa NASA Raila Odinga anasema tume ya IEBC ina muda  wakutosha kutoa upya kandarasi ya kuchapisha karatasi za kupigia kura. Akiongea mjini Mombasa, Raila amepongeza uamzi wa mahakama akisema utahaikisha kandarasi hiyo inatolewa kwa njia ya uwazi. Amesema NASA iko tayari kwa uchaguzi wa Agosti nane na kuwarai wafuasi wao kujiandaa kwa zoezi hilo. Ameitaka IEBC kuzingatia sheria katika utenda kazi wake kuhakikisha hakuna lalama zaidi zinaibuka.

Show More

Related Articles