HabariMilele FmSwahili

Mwili wa Nkaiserry kufanyiwa upusauji katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee

Mwili wa waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Ole Nkaissery utafanyiwa upasuaji kubaini kilichosababisha kifo chake. Nkaissery aliaga dunia mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya kufikishwa katika hosipitali ya karen kwa matibabu. Haikubainika mara moja kilichosababisha kifo chake ikikumbukwa jana alikuwa katika hali nzuri alipohudhuria maombi ya kitaifa katika bustani ya Uhuru park hapa Nairobi. Yakijiri hayo,mkewe waziri wa usalama wa kitaifa Joseph nkaissery, Hellen Nkaissery anaendelea kupokea matibabu katika hosipitali ya Nairobi. Hellen nkaissery ’mama’ kama alivyojulikana amepelekwa hosipitalini humo kutokana na mshtuko wa moyo kufuatia kifo cha ghafla cha mumewe. Mbunge wa kajiado ya kati Memus Ole Kanchori amedhibitisha Bi.Hellena anaendelea kupokea matibabu.

Show More

Related Articles