HabariMilele FmSwahili

Kifo cha Waziri Nkaiserry ni pigo kubwa kwa taifa la Kenya

Waziri wa usalama wa ndani meja jenarali mustaafu Joseph Kasaine Ole Nkaissery ameaga dunia. Nkaissery alifariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Karen hapa Nairobi. Akidhibitisha kifo hicho mkuu wa utumishi wa umma na katibu katika baraza la mawaziri Joseph Kinyua anasema uchunguzi umeanzishwa kubaini kiini hasa cha kifo cha kiongozi huyo. Kifo cha Nkaissery ni pigo kubwa kwa taifa ikizingatiwa mchango wake katika wizara ya usalama wa kitaifa inayotazamwa sana siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu.

Show More

Related Articles