HabariMilele FmSwahili

Donald Trump na Putin wakutana kwa mara ya kwanza Ujerumani

Donald Trump na Vladimir Putin wamekutana kwa mara ya kwanza na wakasalimiana kwa mikono katika mkutano wa G20 mjini Hamburg nchini Ujerumani. Viongozi hao wa marekani na urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa marekani. Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano huo wa siku mbili. Mkewe Trump,Melania trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano yalioshuhudiwa kutwa nzima hapo jana.

Show More

Related Articles