HabariMilele FmSwahili

Je unajua Nkaiserry amekua mwanajeshi kwa Miaka 29 na mbunge kwa Miaka 12

Nkaissery alizaliwa mwaka wa 1949 na amefariki akiwa na umri wa miaka 67. Alichaguliwa waziri wa usalama mwaka 2014 kuchukua nafasi ya Joseph Ole Lenku badaa ya kushuhudiwa misururu ya mashambulizi ya mara kwa mara nchini. Atakumbukwa kwa mageuzi makubwa alioleta katika wizara ya usalama nchini hali iliochangia kupungua mashambulizi kutoka kwa kundi la Al shabab. Nkaissery alijiunga na jeshi mwaka wa 1973 ambapo alipandishwa vyeo kadi kiwango cha major jenerali akihudumu kikosini kwa miaka 29. Alijiunga na siasa mwaka 2002 ambapo alichaguliwa kuhudumu kama mbunge kwa miaka zaidi ya 12.

Show More

Related Articles