HabariMilele FmSwahili

maafisa wakuu serikalini wafika katika chumba cha kuhifadhi maiti cha lee kuuaga mwili wa Nkaiserry

Maafisa wakuu wa serikali,familia na viongozi tofauti wanaendelea kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee ambapo mwili wa waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Ole Nkaissery umepelekwa. Ni baada ya jenerali mstaafu Nkaissery kutangazwa kuaga dunia mwendo wa saa usiku wa kuamkia leo katika hosipitali ya Karen hapa Nairobi. Miongoni mwa waliofika eneo hilo ni aliyekua waziri wa usalama wa kitaifa Joseph ole Lenku ambaye ameelezea kusikitishwa na kifo cha ghafla cha jenerali Nkaissery akitaja kifo hicho kama pigo kubwa sio tu kwa familia,jamii ya wamasaai ila pia kwa taifa. Mbunge wa Rongo Dalmas Otieno aliyekua rafiki wa karibu wa jenerali Nkaissery ametaja kifo chake kama pigo kubwa,usemi mabao umetolewa na mbunge memusi ole kanchori.
kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale ni miongoni mwa waliofika eneo hilo na kuelezea kusikitishwa na kifo cha jenerali Nkaissery.

Show More

Related Articles