HabariMilele FmSwahili

Mwili wa waziri Nkaiserry kufanyiwa upasuaji

Mwili wa waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Ole Nkaissery utafanyiwa upasuaji kubaini kilichosababisha kifo chake. Nkaissery aliaga dunia mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya kufikishwa katika hosipitali ya Karen kwa matibabu. haikubainika mara moja kilichosababisha kifo chake ikikumbukwa jana alionekana akiwa katika hali nzuri alipohudhuria maombi ya kitaifa katika bustani ya Uhuru park hapa Nairobi ambapo alikua ameandamana na rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Show More

Related Articles