HabariMilele FmSwahili

Matiang’i kuhudumu kama kaimu waziri wa usalama

Rais Uhuru Kenyatta amemteua Dr.Fred Matiang’i kuhudumu kama kaimu waziri wa usalama wa kitaifa. Rais Kenyatta anasema amechukua hatua hiyo baada ya kuandaa kikao cha dharura cha baraza la usalama wa kitaifa. Ni uteuzi unaojiri saa chache tu baada ya taifa kuamkia taraifa ya kuaga dunia kwa waziri wa usalama wa kitaifa meja jenerali mstaafu Joseph Ole Nkaissery. Rais Kenyatta amesema hakutakua na pengo lolote katika idara ya usalama wa taifa na kwmaba mikakati imewekwa kuhakikisha shuguli zinaenda sambamba.Rais Kenyatta ambaye amehutubia taifa kutoka ikulu hapa nairobi ameelezea kusikitishwa na kifo cha jenerali mstaafu Ole Nkaissery akisema ni pigo kubwa sio tu kwa taifa ila pia kwa serikali yake.

Show More

Related Articles