HabariMilele FmSwahili

Raila aahidi kuwafidia waliopigania demokrasia iwapo NASA itashinda uchaguzi

Mgombea urais wa NASA Raila Odinga ameahidi kuwafidia viongozi waliopigania demokrasia iwapo NASA itaunda serikali Agosti nane. Raila anazilaumu serikali za awali kwa kuwatelekeza mashujaa hao akisema wengi wamefariki wakiwa maskini licha ya kuchangia demokrasia ya taifa. Akiongea katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamukunji Nairobi,Raila aidha amewarai wakenya kumpa nafasi kuliongoza taifa akihaidi kutekeleza katiba kikamilifu.

Show More

Related Articles