Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

IEBC yamtaka Gavana Joho kuwapa nafasi wapinzani wake

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imemwamrisha gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kuwaruhusu wapinzani wake kuyaweka mabango yao ya kampeni.
Afisa msimamizi wa kituo cha IEBC Mombasa Nancy Kariuki alimuonya gavana Joho kuwa atashtakiwa kulingana na kanuni na sheria za tume ya IEBC iwapo serikali ya kaunti ya Mombasa itaendelea kuwazuia wanasiasa wengine kuweka mabango yao.
Haya yamejiri huku lori la kampeni la mgombea ugavana Mombasa Hassan Omar likiharibiwa na mlinzi kushambuliwa.

Show More

Related Articles