Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mahakama yatupilia mbali zabuni ya Al Ghurair ya kura za rais

Mahakama kuu hii leo imeamrisha kutupiliwa mbali kwa kandarasi ya kuchapisha karatasi za kupigia kura za kiti cha urais, na kuwa pigo kwa tume ya uchaguzi na mipaka.
Kulingana na amri iliyotolewa na majaji watatu na iliyochukua muda wa saa mbili hivi, majaji hao walisisitiza kuwa,kwenye zabuni hiyo , IEBC hawakuwahusisha umma.
Kesii hii iliyokuwa imewasilishwa na muungano wa upinzani NASA, ililenga kufutilia mbali uchapishaji wa karatasi zote za kura zinazochapishwa na kampuni ya Al ghurair kutoka Dubai.
Hata hivyo uchapishaji wa karatasi za viti vingine, utaendelea.

Show More

Related Articles