HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuu yaiagiza IEBC kutoa upya kandarasi ya kuchapisha karatasi za kura

Majaji wa mahakama kuu wameagiza tume ya uchaguzi na mipaka kutoa upya kandarasi ya uchapishaji karatasi za wagobema wa urais. Hii ni baada yao kuamua IEBC haikufuata sheria katika utoaji kandarasi ya moja kwa moja kwa kampuni ya Alghurair . Akitoa uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji watatu, jaji Joel Ngungi amesema IEBC haikuzingatia utaratibu wa sheria katika utoaji kandarasi hiyo.Majaji hao aidha wamesema muda uliosalia unatosha kuhakikisha mchakato huu unaafikiwa ili kuruhusu uchaguzi huru na wa haki.

Show More

Related Articles