HabariMilele FmSwahili

Serikali yatoa shilingi bilioni 12 kwa hazina ya vijana

Serikali  imetoa shilingi bilioni 12 kwa hazina ya vijana fedha zilizotolewa kupitia wizara ya masuala ya vijana na jinsia. Waziri wa vijana Cecil Kariuki anasema shilingi bilioni 9 zimeelekezwa kwa hazina ya  kinamama na kuwafaidi  zaidi ya kina mama milioni 1 na elfu 300. Kariuki amewapa changamoto kina mama na vijana kujitokeza na kutuma maombi ya kupokea fedha hizo ili kubadili maisha yao. Ameongeza kuwa  kufikia sasa  mpango wa huduma kwa vijana wa NYS imefikia maeneo bunge 180 na  kuwafaidi zaidi ya  vijana 150,000.

Show More

Related Articles