HabariPilipili FmPilipili FM News

NASA Washinda Kesi Yakupinga Zabuni Waliopewa Al GHULRAIR

Mahakama ya rufaa jijini Nairobi imesitisha uchapishaji wa karatasi za kura za wadhifa wa urais kwa kampuni ya  Al GHULRAIR ilioko nchini dubai.

Jopo la majaji watatu lililoundwa na jaji mkuu David Maraga limetaka kampuni ya al ghulrair kuendelea kuchapisha karatasi za kura za wagombea wengine wakiwemo,magavana,maseneta,wabunge,wawakilishi wa kina mama na wawakilishi wadi.

Hapo jana mwenyekiti wa IEBC wafula Chebukati alisema kuwa iwapo mahakama itafutilia mbali kandarasi kwa Al ghulrair watakata rufaa.

Show More

Related Articles