HabariPilipili FmPilipili FM News

Wsichana 4000 Wadaiwa Kupachikwa Mimba Ganze.

Mbunge wa   Ganze Peter Shehe amesema kuwa wasichana wadogo zaidi ya 4,000 eneo hilo wamepata mimba.

Akiongea wakati wa siku ya elimu katika shule ya msingi ya Ganze,  Shehe amesema kuwa wahusika wakuu katika kuwatia mimba wasichana hao ni vijana wadogo.

Shehe hata hivyo amesema kuwa wasichana  zaidi ya 4,600 wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka 15 wamepata ujauzito tangu mwaka wa 2013 katika eneo hilo.

Naye mwaniaji wa kiti cha eneo bunge hilo kwa tiketi ya  chama cha ODM Teddy Mwambire amesema kuwa wasichana wengi wamejipata katika hali hiyo baada ya wazazi kupuuza mahitaji yao muhimu wanapovunja ungo.

Teddy amekariri kuwa wasichana wengi wanapovunja ungo hukosa baadhi ya vifaa kama vile taulo za hedhi.

Kauli hiyo hata hivyo imeungwa mkono na afisa wa watoto katika eneo hilo Daniel Mbogo  ambaye ametaja kuwa eneo hilo huripoti kesi  zaidi ya kumi kila mwezi.

 

Show More

Related Articles