HabariPilipili FmPilipili FM News

Bayusuf Aungwa Mkono Na Wapinzani Wake Kuwania Kiti Cha Ubunge Nyali

Wakaazi wa eneo bunge la nyali wametakiwa kutochagua viongozi kwa misingi ya vyama, na badala yake wachague viongozi wenye ruwaza ya kuleta  maendeleo.

Akiongea kwenye kikao na waandishi wa habari mjini Mombasa mwaniaji wa ubunge kwa tiketi ya chama cha jubilee Ashraff Bayusuf amesema wakati umefika kwa wananchi kuwachagua viongozi waadilifu.

Bayusuf ameyasema hayo wakti akiidhinishwa rasmi kuwania kiti hicho na wapinzani wake aliowabwaga kwenye mchujo wa chama cha jubilee.

Kwa pamoja wamemuunga mkono Bayusuf kuwania kiti hicho na wakaapa kuhakikisha anaibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Show More

Related Articles