HabariMilele FmSwahili

Buzeki asema yuko tayari kumuunga mkono Mandago iwapo atashindwa

Mgombea wa ugavana Uasin Gishu Zedekiah Buzeki anasema  yuko tayari kumuunga mkono mpinzani wake  gavana Jackson Mandago iwapo ataibuka mshindi. Buzeki amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kutogawanyika kwenye misingi tofauti kutokana na kinyanganyiro cha ugavana. Anasema ushindi wa yeyote atakayeibuka mshindi  itakuwa ushindi wa wenyeji wa Uasin Gishu. Buzeki  alichukua fursa hiyo  kusalimiana kwa mkono na gavana Mandago ambaye amekuwa mpinzani wake mkuu na kupandisha joto la kisiasa kaunti hiyo.

Show More

Related Articles