HabariMilele FmSwahili

Jaji Maraga awataka mahakimu wote kujiandaa kukabili kesi za uchaguzi

Jaji mkuu David Maraga amewataka mahakimu  kote nchini kujiandaa vilivyo  kukabili kesi  za baada ya uchaguzi wa mwezi Agosti. Anasema mahakimu hao wanastahili kuwa tayari kushughulikia  kesi zitakazotokana na uchaguzi wa waakilishi wadi. Anasema huenda kesi nyingine ambazo si za uchaguzi zikacheleweshwa kwa muda ili kushughulikia kesi  za uchaguzi mkuu.

Show More

Related Articles