HabariPilipili FmPilipili FM News

Gari La Kampeni La Sarai Lavamiwa Mombasa.

Wakazi wa Mombasa wameamkia mshangao mapema leo baada ya watu wasiojulikana kuvamia gari la kampeini za mgombea wa kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Hassan Omar Sarai usiku wa kuamkia leo.

Sarai amekitaja kisa hicho kama njama ya wapinzani wake kumtishia katika kampeini zake, ikiwa ni siku moja tu baada ya kuzindua rasmi msafara wa kampeini hizo.

Hata hivyo amesema hatishwi na vitendo vya baadhi ya wanasiasa wanaotumia njia za kihuni kutaka kuingia mamlakani, na kuitaka serikali kuu kuimarisha usalama kwa wagombea wote na wananchi kwa ujumla.

Show More

Related Articles