BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Susumila Hanitishi Kwenye Uimbaji Asema Chikuzee

Msanii chikuzee amejitokeza wazi nakusema wasanii ambao wanamtisha kwa sana kutoka Mombasa si Susumila, Ally B wala Nyota Ndogo bali ni Shembwana Masauti na Kigoto.

Akiwa katika mahojiano kwenye kipindi cha MwakeMwake Live msanii chikuzee amebainisha wazi kuwa wasanii wanaomtisha ni shembwana na kigoto na hataki wazembee katika uimbaji wao.

Akiulizwa kuhusu Susumila Chiku amesema wasanii ni wengi lakini hawa wawili ndio wanampa kichwa kuuma kwani wanajua kuimba tatizo ni kuwa wamelaza maskio yao.

“Wasanii ni wengi Mombasa ila hawajatia bidii na hilo ndo lanifanya niwe juu yao lakini wakianza kuporomosha nyimbo watanitishia”. Amesema Chikuzee

Wakati huohuo meneja wa Chikuzee Musa Babaz amesema kama kuna msanii anayejua kuimba kuliko Chikuzee ajitokeze atamsaidia kwenye uimbaji wake na atampeleka Tanzania kurekodi mziki wake

Show More

Related Articles

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker