HabariMilele FmSwahili

Chebukati: Hatutaipokonya kandarasi ya Alghurair

Kandarasi ya kuchapishwa karatasi za kura haitapokonywa kampuni ya Al ghurair licha ya tetesi zinazotolewa na upinzani. Mwenyekiti Wafula Chebukati anasema upinzani haujatoaa ushahidi wowote kuhusiana na madai IEBC ilishawishiwa na maafisa wa ikulu ya rais kuipa kampuni ya Alghurair kandarasi ya uchapishaji karatasi za kupigia kura. Akizungumza baada ya mkutano na wagombea rais hapa Nairobi,Chebukati anasema lengo la mkutano huo ilikuwa kuwafahamisha kuhusu sababu zilizopelekea kuchaguliwa kwa kampuni ya Al ghurair. Amewahakikishia suala hili halitahujumu uchaguzi mkuu. Licha ya hakikisho hilo wagombea hao wameshtumu IEBC kwa kupendelea muungano wa nasa.naye gavana wa kaunti ya nairobi Dkt Evans Kidero amepuuzilia mbali wito wa Chebukati kuwataka wanasiasa na wadau wengine kuelekea Dubai kushuhudia uchapishaji wa karatasi hizo ili kuondoa utata uliopo.

Show More

Related Articles