HabariMilele FmSwahili

Kocha wa Gor Mahia ajiuzulu

Kocha wa Gor mahia Jose Marcelo Feraira ukipenda Ze Maria amejiuzulu kama kufunzi wa klabu hiyo.

Inakisiwa kwamba zimaria amegura klabu hiyo baada ya uongozi wa klabu hiyo kutotimiza ahadi walizomwahidi.

Ze maria aliteuliwa kuwa kocha wa kogalo mwezi machi mwaka jana , baada ya frank nuttal kujiondoa . ze maria aliongoza gor mahia kumaliza nambari mbili kwenye jedwali la ligi kuu msimu jana nyuma ya mabingwa tusker. Alishinda kombe la DSTV super cup mapema mwaka huu baada ya kuwapiga tusker na pia aliiongoza gor mahia wikendi iliyopita kubeba dimba la super cup nchini Tanzania.

Show More

Related Articles