HabariPilipili FmPilipili FM News

Mvurya Amsuta Makwere Kwale.

Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya na naibu wake Fatuma Achani wamemsuta mgombea wa  ugavana kwale kwa tiketi ya chama cha WIPER  Ali Chirau Mwakwere kwa madai ya kupanga njama ya kuvuruga mikutano yao ya  kisiasa na ufunguzi wa miradi  ya jamii.

Wakizungumza katika ufunguzi wa afya house uliofanyika katika uwanja wa baraza park mjini Kwale wawili hao wamesema Mwakwere anadaiwa kuunda makundi ya vijana kuvuruga  ufunguzi huo .

Aidha wamemtaka mgombea huyo  kutafuta kiti hicho kwa kuuza sera badala ya kuleta uchochezi na chuki katika jamii ya wakwale.

Show More

Related Articles