HabariMilele FmSwahili

Shughuli za uokozi katika orofa iliyoporomoka Kware zaendelea

Shughuli za uokoaji zinaendelea wakati huu katika eneo la Kware mtaani Embakasi hapa Nairobi kufuatia kuporomoka jumba la orofa 7 usiku wa kuamikia leo.Idara ya majanga inashirikana na wanajeshi kuendesha uwokozi huo baada ya kuhofiwa huenda takriban watu 15 wamefunikwa na vifusi  vya jengo hilo. Hata hivyo hakuna maafa yaliyoripotiwa.Yakijiri hayo,serikali ya kaunti ya Nairobi imejitenga na kuidhinisha jumba hilo, gavana Evans Kidero akisema hakufahamu ujenzi huo uliendeshwa kinyume na sheria

Show More

Related Articles