HabariMilele FmSwahili

Bunge la seneti kurejelea vikao vyake leo

Bunge la seneti linarejelea vikao vyake leo baada ya likizi ya miezi miwili. Bunge hilo litakuwa na vikao vitatu pekee kabla ya kufungwa rasmi kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Ajenda kuu katika vikao hivi itakuwa kuidhinishwa ripoti ya kamati ya fedha kuhusu mswada wa ugavi wa mapato ambao umezua utata. Bunge la seneti na la kitaifa zimekosa kuafikiana kuhusu pendekezo la seneti kuwa mgao unaokabidhiwa serikali za kaunti uongezwe kwa zaidi ya shilingi bilioni 29. Aidha bunge la kitaifa liliidhinisha kaunti kukabidhiwa Shilingi bilioni 291 badala ya 323 zilizopendekezwa na tume ya ugavi wa mapato.

Show More

Related Articles