HabariPilipili FmPilipili FM News

Machifu Waunda Kamati Ya Kuhubiri Amani.

Machifu katika eneo bunge la  Wundanyi kaunti ya Taita Taveta,wamebuni kamati maalum za kuangazia usalama katika maeneo yao ya uwakilishi , sawa na kushinikiza umoja na amani, wakati huu taifa linapoendelea kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu.

Wakiongozwa na Solomon Kilambo machifu hao wamesema agenda yao kuu ni kushinikiza umoja na amani huku wakilenga kutoa hamasa kwa vijana ambao wakati mwingi ndio hutumiwa kuzua vurugu na wanasiasa.

Aidha  Machifu hao wamewataka washikadau wote kushirikiana kikamilifu  ili kuona kila mwananchi anaishi kwa amani kabla, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Show More

Related Articles