HabariPilipili FmPilipili FM News

Feri Mpya Kuwasili Nchini Mwezi Ujao.

Halmashauri ya Huduma za Ferry nchini imesema Feri Mpya ijulikanayo kama Mv Jambo iliyotengenezewa nchini Uturuki itawasili nchini tarehe 27 Mwezi Ujao tayari kuanza rasmi huduma katika kivuko cha Likoni.

Mkurugenzi Mkuu wa halmashauri hiyo Bakari Gowa amesema Ferry hiyo iliyozinduliwa Rasmi nchini Uturuki kwenye sherehe ilizohudhuriwa na maafisa wakuu wa serikali kutoka humu nchini inatarajiwa kuanza safari yake tarehe 6 Julai kuja mjini Mombasa.

Gowa amesema kwamba anaimani kuwa wananchi wanaotumia kivuko cha ferry cha Likoni watanufaika na huduma za feri hiyo itakapowasili humu nchini.

Kulingana na Gowa Fery hiyo mpya iko na urefu wa mita 84.6,upana wa mita 18 na itakuwa na uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,534.

Hii ni mojawapo ya Feri  Mbili Ambazo serikali ya Kenya Imeagiza kutoka Uturuki kwa Kima cha shilingi Billioni 2.2.

Show More

Related Articles